Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirika la habari la FARS limemnukuu Saeed Khatibzadeh akisema hayo kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuongeza kuwa, Marekani haijali kuweka vikwazo vipya hata katikati ya mazungumzo ya Vienna.
Amesema, Washington haiwezi kuelewa kwamba siasa zake za vikwazo vya kiwango cha juu haziwezi kulipigisha magoti taifa kubwa la Iran bali pia zinakwenda kinyume na madai ya kutumia udiplomasia kutatua matatizo. Ameongeza kuwa, kuongeza vikwazo si tu hakuisaidii Marekani, lakini pia kunakwenda kinyume na madai ya Washington ya kuwa na nia njema.
Jana Jumanne, Wizara ya Hazina ya Marekani iliendeleza uadui wa nchi hiyo ya kibeberu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuwaweka kwenye orodha yake ya vikwazo watu wanane na taasisi nne za Kiirani.
Vikwazo hivyo vipya vimewekwa dhidi ya Iran katika hali ambayo rais wa Marekani, Joe Biden anadai kuwa ana nia ya kutatua matatizo yaliyopo kwa njia ya mazungumzo yanayoendelea hivi sasa mjini Vienna, Austria.
Wakuu wa serikali ya hivi sasa ya Marekani wamekuwa wakikiri mara kwa mara kuwa, siasa za Washington za vikwazo vya kiwango cha juu kupindukia dhidi ya Iran zimefeli. Wamekuwa wakidai pia kuwa Marekani ina nia ya kurejea kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA lakini hadi hivi sasa hawajaonesha nia yoyote njema katika suala hilo.
342/